YANGA WAENDELEZA JUHUDI ZA UJENZI WA UWANJA

Na,Said Ally
Uongozi wa klabu ya Yanga umeonekana kudhamiria kuhakikisha kuwa klabu hiyo inafanikiwa kuwa na uwanja wake wa mazoezi kutokana na juhudi kubwa ambazo wanaendelea kuzifanya katika ujenzi wa uwanja huo uliopo makao makuu ya klabu hiyo maeneo ya Jangwani.
Kwa sasa zoezi ambalo linaendelea kwenye uwanja huo ni umwagaji wa vifusi jambo ambalo MWANDIKE.BLOGSPOT limeshuhudia likienda vizuri kwa kiwango kikubwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa uongozi wa klabu hiyo zinasema kwamba lengo lao ni kuhakikisha klabu inakuwa na uwanja wake wa mazoezi na ikiwezekana baadhi ya mechi za kirafiki zichezwe katika uwanja huo.

No comments