KUKUTWA NA DAWA ZA KUPUNGUZA NGUVU MICHEZONI NI KOSA LA JINAI

Na,Said Ally
Mwenyekiti wa chama cha wataalamu wa tiba za wanamichezo Tanzania (TASMA) Mwanandi Mwankema amesema kwamba ni vigumu sana kupatikana kwa dawa za kupunguza nguvu kwa wachezaji michezoni licha ya taarifa hizo kuelezwa na wadau kuwa vilabu vingi vimekuwa vikitumia mbinu hiyo ili kupata ushindi.

Mwankema ameiambia MWANDIKE.BLOGSPORT kuwa dawa ambazo zinatumika hasa katika kuleta usingizi ama kumpunguza nguvu mchezaji ni dawa ambazo zinahifadhiwa Hospitalini na zina sheria yake maalumu katika utoaji.

Alisema kwamba dawa hizo huwa zinatumika kwa ajili ya wagonjwa kwa matumizi mbalimbali kama kumfanya mgonjwa apate usingizi na matibabu mengine ambapo utolewaji wake hadi kuwepo kwa saini ya maofisa watatu.

Aidha alisema kwamba mtu atakaekutwa na dawa hizo nje ya Hospitali ni kosa la jinai ambapo anapaswa kuhukumiwa mahakamani.

Hata hivyo Mwandandi alisema kwamba wadau na viongozi wa vilabu wanapaswa kufahamu kuwa hizo kauli ambazo zinatolewa kuwa kuna vilabu vinatumia dawa hizo bado hakuna uthibitisho wowote ispokuwa baadhi ya timu zinatumia mbinu mbadala ili kuwatoa wapinzani wao mchezoni.

No comments