KOCHA SIMBA ASEMA KIKOSI CHAKE KIPO TAYARI KUWAVAA AL MASRY


Na Said Ally
Kocha mkuu wa timu ya Simba Pierre Lechantre amesema kwamba kikosi chake kinataraji kushuka dimbani hapo kesho kikitambua kuwa watakuna na upinzani mkali kutoka kwa wapinzani wao lakini kwao wamejipanga kushinda.

Lechantre alisema kwamba anaifahamu vizuri Al Masry ambayo kwa sasa inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi nchini Misry nchi ambayo ameeleza kuwa huwa ina timu bora zenye ushindani.

Aidha alisema kwamba wanachama na mashabiki wanapaswa kufahamu kuwa kwa upande mmoja kuna Simba na pia upande mwingine kuna Al Masry hivyo lolote katika mchezo huo linaweza kutokea hasa kwa vijana wake wa Simba kuibuka na ushindi.

Kwa upande wake nahodha wa Simba John Bocco yeye alisema kwamba kwa upande wao kama wachezaji wamejipanga kikamilifu na pambano hilo hivyo ni vyema wanachama na mashabiki wakajitokeza kwa wingi uwanjani hapo kesho.

Bocco aliongeza kwa kusema kwamba watanzania wanapaswa kufahamu Simba inaiwakilisha nchi kwenye michuano hiyo ya kimataifa hivyo ni vyema nguvu zao zote wakazielekeza katika mechi hiyo itakayopigwa kwenye uwanja wa taifa kuanzia mishale ya saa 12 na jioni.

No comments