LIPULI FC WAKO TAYARI KUWAVAA MAJIMAJI

Na Said Ally
Uongozi wa timu ya soka ya Lipuli FC,umesema kwamba kikosi cha timu hiyo kimejiandaa vyema kuwakabili Majimaji FC hapo kesho katika mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Msemaji wa timu hiyo Clement Sanga amesema kwamba wachezaji wote 20 ambao wamesafiri na timu ukiondoa Jerome Rambele wote wapo katika hali nzuri ya pambano hilo litakalopigwa Mjini Songea.

Sanga alisema kwamba kuelekea kwenye pambano hilo atakosekana mchezaji Jerome Rambele ambae yeye atakosekana baada ya mchezaji huyo kufiwa na baba yake mzazi.

Alisema kwamba Jerome leo hii ameanza safari ya kuelekea Kigoma kwa ajili ya kushiriki mazishi ya baba yake mzazi na kama uongozi pamoja na wachezaji wamejipanga kikamilifu kupata ushindi kwenye pambano hilo ambao utamfariji mchezaji huyo.

No comments