WAPINZANI WA SIMBA WAWASILI NCHINI

Timu ya Al Masry kutoka nchini Misri imewasili leo hii asubuhi jijini Dar es salaam tayari kwa ajili ya mchezo wao wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya vinara wa ligi kuu ya Tanzania bara Simba hapo siku ya jumatano.

Baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,Al Masry walitumia basi la Azam FC kuwapeleka katika hotel ambayo wamefikia.

Kikosi hicho kinatarajiwa kufanya mazoezi hapo kesho katika uwanja wa Taifa kwa ajili ya maandalizi ya mwishomwisho kuelekea pambano hilo litakalopigwa kuanzia mishale ya saa 12 jioni.

No comments