FULL TIME, SIMBA 2-2 AL MASRY

Mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika kati ya Simba SC dhidi ya Al Masry ambao ulisimama kwa muda kuanzia dakika ya 85 kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Uwanja wa Taifa na kupelekea umeme kupata hitilafu uwanjani hapo umemalizika kwa dakika 90 kwa timu hizo kutoshana nguvu ya kufungana mabao 2-2.

Mechi hiyo ililazimika kusubiliwa kwa muda kuendelea kwa dakika ambazo zimesalia baada ya taa za uwanja wa Taifa kupata hitilafu kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hali ambayo iliwalazimu wahusika kulitatua tatizo hilo kwa haraka.

Mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani wa hali ya juu uliharibiwa na mvua kubwa ambayo ilinyesha uwanjani hapo na kusababisha kupoteza radha ya mchezo wakati timu ziliporejea uwanjani baada ya swala la umeme kushughulikiwa.

Katika mtanange huo magoli ya Simba yamefungwa na John Bocco na Emlmanuel Okwi  yote kwa mikwaju ya penati wakati magoli ya Al Masry yamefungwa na Ahmed Gomaa na Ahmed Shoukry. 

No comments