TETESI ZA SOKA ULAYA LEO IJUMAA

Mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane, mwenye umri wa miaka 24 ameamua kusalia katika klabu ya Tottenham kwa zaidi ya msimu mmoja lakini timu hiyo bado inakabiliana na ugumu wa kumbakiza mlinzi wa kati raia wa Ubelgiji Alderweireld, na mlinzi wa kushoto Danny Rose, ambao wote wanawaniwa na Manchester United.
Kane anatarajiwa kuwa nahodha wa timu ya Uingereza katika michuano ya kombe la dunia akishirikiana na Jordan Henderson pamoja na Gary Cahill.
Miamba ya soka ya Ufaransa Paris St-Germain inamtaka Antonio Conte kuwa meneja wao.
Vinara hao wa The Ligue 1 wanamnyatia pia meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino.
Mabosi wa Manchester United wanamuunga mkono meneja wa klabu hiyo Jose Mourinho na watawapiga bei wachezaji wote wasioendana na mfumo wa mreno huyo.
Klabu za Chelsea na Real Madrid zinaongoza mbio za kumuwania mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski raia wa Poland mwenye miaka ya 29 ambaye yuko mguu ndani mguu nje.
Klabu ya Chelsea inapewa kipaumbele cha kunasa saini ya mlinzi wa Napoli, raia wa Senegal Kalidou Koulibaly mwenye umri wa miaka 26 anayewaniwa pia na klabu ya Arsenal na Manchester.
Barca watachuana na mahasimu wao, Real Madrid kumsajili beki wa pembeni mwenye asili ya Austria anayekipiga na Bayern Munich, David Alaba (25).
Mabingwa wa nchini Ujerumani, Bayern wamejiunga na Arsenal na Tottenham kumuwania kiungo mshambuliaji raia wa Brazil Malcom mwenye miaka 21 kutoka kikosi cha Bordeaux.
Arsenal,Leicester na Southampton wanafikiria kumsajili Mohamed Elyounoussi wa Basel.Mshambuliaji huyo, 23, raia wa Norway alifunga goli dhidi ya Manchester City katika ligi ya mabingwa siku ya Jumatano.

No comments