MARIGA AITWA TIMU YA TAIFA YA KENYA

Kiungo mkongwe wa Kenya, MacDonald Mariga ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya, Hareambee Stars chenye wachezaji 24 kitakachocheza mechi mbili za kimataifa kwa mujibu wa kalenda ya Fifa. 

Kenya inayofunzwa na kocha wa muda Stanley Okumbi itachuana na Comoro na Jamhuri ya Afrika ya Kati katika mechi za kimataifa zilizo kwenye kalenda ya FIFA.

Mariga anayechezea klabu ya Real Oviedo ya Hispania anaitwa kwenye kikosi cha Kenya baada ya kukosekana kwa miaka mitatu tangu alipoichezea Harambee Stars kwa mwara ya mwisho mwaka 2015. Sanjari na Mariga pia Kocha Mkuu wa Kenya amemuita mdogo wake Mariga, Victor Wanyama ambaye anaichezea klabu ya Tottenham Hotspurs ya Uingereza.

Nyota wengine waliojumuishwa kwenye kikosi hicho ni Francis Kahata anayechezea Gor Mahia na Paul Were anayechezea FC Kaisar ya Kazakhstan.

Kikosi kamaili ni kama ifuatavyo

Makipa ni Patrick Matasi, John Oyemba na Faruk Shikalo.

Walinzi ni Harun Shaka, Brian Manderla, David Ochieng, David Owino, Abud Omar.

Viungo walioitwa ni Patilah Omoto, Francis Kahata, Duncan Ochieng, Samuel Onyango, Athuman Ismail Gonzales, Antony Akumu, Victor Wanyama, McDonald Mariga, Johanna Omollo, Paul Were na Erick Omond.

Washambuliaji walioitwa kikosini ni Jesse Were, Cliffton Miheso, Erick Kapaito, Michael Olunga na Ayub Timbe.

No comments