WACHEZAJI WATANO WA ZANZIBAR WAITWA TAIFA STARS

Na Said Ally
Nyota wa Tanzania wanaocheza Mpira wa kulipwa nje ya nchi wameitwa kwenye kikosi cha Timu ya Tanzania Taifa Stars kitakachokuwa na jumla ya Wachezaji 23 ambao wanataraji kuingia kambini Machi 18 mwaka huu kwenye Hotel ya SeaScape iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza safari machi 19 kuelekea nchini Algeria.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Kocha msaidizi wa Timu ya Tanzania Taifa Stars Hemed Morroco amesema  katika kalenda ya FIFA Taifa Stars itakuwa na mechi mbili za kirafiki ambayo moja ni dhidi ya Algeria itakayochezwa nchini Algeria Machi 22 mwaka huu na nyingine ni dhidi ya DR Congo itakayochezwa Machi 27 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Katika kikosi hicho Morroco amewajumuisha wachezaji watano kutoka Zanzibar akiwemo kiungo mahili Faisal Salum.

Wachezaji 23 walioitwa ni:- 
WALINDA MLANGO 
1. Aishi Manula 
2. Ramadhan Kabwili 
3. Abdulrahman Mohammed 

WALIZNI 
1. Shomari Kapombe 
2. Hassan Kessy 
3. Gadiel Michael 
4. Kelvin Yondani 
5. Abdi Banda 
6. Erasto Nyoni 

VIUNGO
1. Hamis Abdallah 
2. Mudathir Yahaya 
3. Said Ndemla 
4. Faisal Salum 
5. Abdulazizi Makame 
6. Farid Mussa 
7. Thomas Ulimwengu
8. Ibrahim Ajib 
9. Shiza Kichuya 
10. Mohammed Issa 

WASHAMBULIAJI 
1. Mbwana Samatta 
2. Saimon Msuva 
3. John Bocco 

4. Yahaya Zayd

No comments