TFF YASISITIZA SIMBA NA YANGA KUCHEZA UWANJA WA UHURU

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limesema kwamba mchezo wa watani wa Jadi Simba na Yanga utachezwa katika uwanja wa Uhuru uliopo jijini Dar es salaam kama ilivyopangwa hapo awali.

Afisa Habari wa TFF,Alfred Lucas amesema kwamba mchezo huo unaotarajiwa kupigwa siku ya jumamosi ya tarehe 28 ya mwezi huu utachezwa kwenye uwanja huo wa Uhuru licha ya baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kwamba huenda ungezwa kwenye uwanja wa Taifa.

Lucas alisema kwamba TFF imeheshimu maamuzi ya wamiliki wa uwanja ambao awali walitoa taarifa kua uwanja huo utakamilika kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu ili kuufanya uwanja huo uwe bora zaidi.

Aidha shirikisho hilo limetangaza viingilio vya mchezo huo wa watani wa jadi Simba na Yanga ambapo kiingilio cha chini ni shilingi elfu 10000 huku kiingilio cha juu kikiwa shilingi elfu 20000.

No comments