TFF YATANGAZA MWISHO WA UUZWAJI WA TIKETI ZA SIMBA NA YANGA

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limetangaza kuanza mchakato wa uuzwaji wa tiketi za pambano la watani wa jadi Simba na Yanga linalotarajiwa kuchezwa agost 28 mwaka huu katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Afisa Habari wa TFF,Alfred Lucas ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT.COM kwamba tiketi hizo zimeanza kuuzwa kuanzia leo hii kwa njia ya mtandao ambapo kiingilio cha chini ni shilingi elfu 10,000 huku kiingilio cha juu kikiwa elfu 20,000

Lucas alisema kwamba tiketi hizo zitauzwa hadi siku ya ijumaa ya tarehe 28,siku moja kabla ya mchezo na hakutakua na mauzo ya tiketi siku yenyewe ya mchezo huo hapo jumamosi.

Alisema kwamba nivyema mashabiki na wadau wa soka wakanunua mapema tiketi hizo ili kuondoa usumbufu ambao huenda ukajitokeza kuelekea kwenye pambano hilo lililokua gumzo kwa sasa.

Mashabiki wengi wana shauku ya kulitazama pambano hilo hivyo itawalazimu kununua mapema tiketi za mchezo huo ili kupata nafasi ya kuingia kwenye uwanja huo unaotarajiwa kuingiza mashabiki elfu 23,0000.

No comments