AZAM FC WAPO KAMILI KUWAVAA MBEYA CITY


Uongozi wa klabu ya Azam FC,umesema kwamba kikosi chao kimejipanga vyema kuwakabili Mbeya City hapo kesho katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara utakaopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi.

Msemaji wa Azam FC,Jafary Idd ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT.COM kwamba baada ya kurejea kanda ya ziwa kikosi cha timu hiyo kiliingia kambini moja kwa moja kwa ajili ya kujiwinda na pambano hilo litakalopigwa kuanzia mishale ya saa moja usiku.

Jafary alisema kwamba wachezaji wote wako vizuri kuelekea kwenye mchezo huo hivyo ni jukumu la benchi la ufundi kumpanga mchezaji watakaemuona anafaa kwa ajili ya mchezo huo.

Alisema kwamba dhamira yao ni kupata ushindi kwenye mchezo huo ili wajiweke kwenye mazingira mazuri katika jitihada zao za kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara msimu huu.

No comments