YANGA WAWASILI DAR ES SALAAM KUWAVAA SIMBA

Kikosi cha timu ya Yanga tayari kimeshawasili jijini Dar es salaam kikitokea mkoani Morogoro tayari kwa maandalizi ya mwisho ya kujiwinda na mchezo wao wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya mahasimu wao wa jadi Simba.

Baada ya kuwasili jijini Dar es salaam kikosi hicho kilielekea katika Hotel ya Protea iliyopo maeneo ya Oysterbay kwa ajili ya kuweka kambi kabla ya hapo kesho kuwavaa wekundu wa Msimbazi Simba.

No comments