MBARAKA YUSUPH ABEBA TUZO YA MCHEZAJI BORA

Mshambuliaji Mbaraka Yusuph, ndiye Mchezaji Bora wa Azam FC (NMB Player of the Month) mwezi Septemba.
Yusuph ametwaa tuzo hiyo baada ya kupigiwa kura nyingi na mashabiki wengi wa soka na kuwazidi wapinzani wake waliokuwa wakishindanishwa naye, kipa Razak Abalora na kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’.
Jumla ya kura 358 zilipigwa kwenye akaunti rasmi za Azam FC za mitandao ya kijamii ya facebook na instagram, zilizowagusa wachezaji hao watatu waliokuwa waikipiga kura.
Mshambuliaji huyo akapata takribani asilimia 65 ya kura hizo zote baada ya kuibuka kidedea kwa jumla ya kura 190, akipigiwa 140 kwenye facebook na zile za Instagram zikiwa 50.
Abalora ameshika nafasi ya pili akizoa jumla ya kura 86, akipata kura 59 facebook na 27 instagram huku Sure Boy akipigiwa jumla ya kura 82 (facebook 65, instagram 17).

No comments