SIMBA WAREJEA DAR ES SALAAM WAKIWA NA TAMBO YA KUIFUNGA YANGA

Na,Suleiman Ussi
Kikosi cha timu ya Simba tayari kimesharejea jijini Dar es salaam kikitokea Zanzibar kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya mahasimu wao Yanga.

Akizungumza na MWANDIKE. BLOGSPOT. COM wakati wakianza safari ya kurejea jijini Dar es salaam,mkuu wa idara ya habari na mawasiliwano wa klabu ya Simba,Haji Manara alisema kwamba hali ya kikosi ipo vizuri na kesho wanachama na mashabiki wa Simba wanapaswa kujitokeza uwanjani ili kushuhudia Yanga atakavyofungwa.

Aliongeza kusema kwamba Simba ina kikosi bora kuliko Yanga,hivyo anaamini ushindi kwao kesho ni jambo la kawaida katika mechi hiyo itakayopigwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Kikosi cha Simba baada ya kuwasili jijini Dar es salaam,kilielekea Serena Hotel kwa ajili ya kuweka kambi kabla ya kuwavaa wapinzani wao Yanga ambao kikosi chao kiliweka kambi mkoani Morogoro.

No comments