KAMATI YA WAAMUZI YAMTANGAZA MWAMUZI WA MECHI YA SIMBA NA YANGA

Mwenyekiti wa  kamati ya waamuzi ya shirikisho la soka nchini,Salum Umande Chama amemtangaza Elly Sassi kua ndie mwamuzi atakaechezesha pambano la watani wa jadi Simba na Yanga litakalopigwa agost 28 mwaka huu kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Chama alisema kwamba kamati hiyo imeamua kumpa jukumu Sassi kuchezesha pambano hilo kutokana na ubora wake ambao ameendelea kuuonyesha katika mechi mbalimbali za ligi.

Sassi ambae hilo litakua pambano lake la pili kuchezesha mechi ya watani wa jadi ni miongoni mwa waamuzi bora ambao msimu uliopita alifanikiwa kubeba tuzo ya mwamuzi bora wa msimu.

No comments