SIMBA YAWASILI ZANZIBAR KUWAVUTIA KASI YANGA

Na Sleiman Ussi,Zanzibar
Kikosi cha timu ya Simba tayari kimewasili Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi ya kujiwinda na pambano la ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya mahasimu wao wa jadi Yanga.

Mratibu wa Simba,Abas Ally ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT.COM kwamba wachezaji 24 ndio waliowasili Zanzibar kwa ajili ya pambano hilo linalotarajiwa kuwa na upinzani wa hali ya juu.

Abasi alisema kwamba hadi kufikia sasa hawana taarifa kamili kama watacheza mchezo wa kirafiki na moja ya timu kutoka hapo Zanzibar hadi uongozi utakapoweka bayana juu ya swal ahilo.

Alisema kwamba kikosi cha Simba kitakaa Zanzibar kwa muda wa wiki moja na kitarajea Dar es salaam siku ya mchezo husika.

Nae kocha msaidizi wa timu ya Simba,Massoud Djuma kwa upande wake alisema kwamba wachezaji wote wa Simba ambao wamewasili Zanzibar wako salama kwa ajili ya maandalizi hayo.

No comments