YANGA KUREJEA DAR ES SALAAM KWA BASI

Kikosi cha timu ya Yanga hapo kesho kinataraji kuanza safari ya kuelekea jijini Dar es salaam kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Simba.

Msemaji wa timu ya Yanga,Dismas Ten ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba baada ya mchezo wao wa jana dhidi ya Stend United kikosi kilisali mkoani Shinyanga na leo hii kimefanya mazoezi mkoani humo.

Dismas alisema kwamba kwa mujibu wa uongozi wa timu,kikosi baada ya kuwasili jijini Dar es salaam hakitaenda nje ya mji kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo labda kuwepo na mabadiliko.

Aidha Dismas amewaomba wanachama wa klbu hiyo ya Yanga kuendelea kutoa hamasa ya kutosha kwa wachezaji ili wafanikiwe kupata matokeo mazuri katika ligi ikiwemo mchezo wao dhidi ya Simba hapo siku ya jumamosi.

No comments