YANGA YAANZISHA TIMU YA WANAWAKE


Uongozi wa klabu ya Yanga umeanzisha rasmi timu ya wanawake ya mpira wa miguu itakayojulikana kwa jina la Yanga Princess.

Mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu ya Yanga pia akiwa makamu mwenyekiti wa kamati itakayosimamia timu hiyo,Siza Lyimo alisema kwamba zoezi la kujisali kwa wachezaji wa timu hiyo limeanza rasmi leo hii octoba 25 hadi hapo 31 mwezi huu.

Siza alisema kwamba zoezi la kupata wachezaji wa timu hiyo litaongozwa na katibu mkuu wa Yanga,Charse Boniphace Mkwasa kutokana na ujuzi wake wa ufundishaji mpira.

Aidha Siza alisema kwamba kamati ya mashindano kwa soka la wanawake ndani ya klabu ya Yanga itaundwa na wajumbe 12 huku mwenyekiti wa kamati akiwa Hawa Ghasia ambae ni Mbunge.

Hata hivyo amewataka wachezaji watakaojitokeza katika mchakato huo kuwa na mapenzi mema na Yanga kwani dhamira yao ni kuona hakutakuwa na mchezaji wa kuhama hama.

No comments