KOCHA SIMBA AWAAMBIA MASHABIKI WASITEGEMEE MAAJABU

Kocha msaidizi wa timu ya Simba,Djuma Massoud amewaambia mashabiki wa timu hiyo wasitegemee kuona maajabu ndani ya kikosi hicho kutokana na ujio wake.

Massoud alisema kwamba katika mpira kuna mambo matatu ya kushinda,kufungwa na kutoa sale hivyo mashabiki hawapaswi kua na dhana ya moja kwa moja kua huenda akaleta maajabu makubwa katika timu.

Alisema kwamba yeye atahakikisha anatumia ujuzi wake alio nao kuwafundisha wachezaji akishirikiana na benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Joseph Omog ili kuhakikisha Simba inapata mafanikio.

No comments