HAJI MANARA AMSIFU KOCHA WA YANGA

Mkuu wa idara ya Habari na mawasiliano wa klabu ya Simba,Haji Manara amemmwagia sifa kocha mkuu wa klabu ya Yanga,George Lwandamini akisema kwamba ni miongoni mwa makocha bora wenye uwezo wa kusoma mchezo.

Manara ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT.COM,kwamba Lwandamina alikuwa kikwazo kikubwa kwa timu yake ya Simba kushindwa kupata ushindi katika mchezo wao uliomalizika kwa suluhu ya kufungana bao 1-1,kwani alikipanga kikosi chake kwa ustadi mkubwa.

Alisema kwamba mbinu aliyoitumia ya kupaki basi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza ilikuwa kikwazo kikubwa kwao hasa baada ya wachezaji wake kuumudu vizuri mfumo huo uliyowabana Simba kushindwa kutamba katika mchezo huo.

No comments