TFF,YASEMA SIMBA NA YANGA ZIMEPATA HASARA
Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limesema kwamba mchezo uliowakutanisha Simba na Yanga siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam umeleta athari kubwa kwa timu za Simba na Yanga kutokana na idadi ndogo ya mashabiki walioingia uwanjani.
Mjumbe wa kamati ya utendaji wa TFF kupitia kanda ya Dar es salaam,Lameck Nyambaya ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT.COM,kwamba idadi ndogo ya mashabiki imesababisha timu hizo kukosa mapato mengi ya uwanjani.
Nyambaya alisema kwamba anaamini gharama ambazo zimetumika kwa timu zote mbili ni kubwa kuliko mgawo walioupata kupitia mchezo huo uliomalizika kwa suluhu ya kufungana bao 1-1.
Alisema kwamba kwa upande wao TFF walitegemea kuona idadi kubwa ya mashabiki kuingia uwanjani hasa kutokana na udogo wa kiwanja cha Uhuru lakini jambo hilo limekwenda tofauti.
Hata hivyo Nyambaya aliwataka mashabiki kuendelea kujitokeza kwa wingi viwanjani ili kuzipa hamasa timu zao na pia zipate pesa za kujikimu kupitia viingilio vyao.

Post a Comment