PAMBANO LA SINGIDA UNITED NA YANGA LASIMAMISHA SHUGHULI ZA WAKAZI WA SINGIDA

Mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara kati ya Singida United dhidi ya Yanga unaotarajiwa kupigwa leo hii katika uwanja wa Namfua mkoani Singida unatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na hamasa iliyopo kwa mashabiki wa mkoa huo na mikoa jirani

Idadi kubwa ya mashabiki mapema tu leo hii asubuhi wamejitokeza kukata tiketi kwa ajili ya pambano hilo la ligi kuu ya Tanzania bara ambao wengi wao wamesimamisha shughuli zao ili kushuhudia pambano hilo litakalopigwa kuanzia mishale ya saa 10 kamili jioni.
Singida United inarejea katika uwanja wake wa nyumbani kwa mara ya kwanza baada ya uwanja huo kuwa katika ukarabati huku mabingwa watetezi wa ligi hiyo wanarejea kwenye uwanja huo baada ya miaka 17 iliyopita ambapo timu hizo zilipokutana Yanga ilikubali kichapo cha bao 1-0.

Kwa mujibu wa uongozi wa klabu ya Singida United umeeleza kwamba kiingilio cha chini ni shilingi elfu 7000 huku kiingilio cha juu kikiwa shilingi elfu 10000.

No comments