SINGIDA UNITED WASEMA HAWANA UNDUGU NA YANGA

Uongozi wa timu ya Singida United umelaani vikali kauli ambazo zinatolewa na baadhi ya wadau wa soka wanaosema kwamba klabu hiyo ina undugu na timu ya Yanga.

Katibu mkuu wa Singida United,Abdulrahman Sima ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT.COM kwamba uongozi unakemea vikali taarifa hizo,hivyo wadau wanapaswa kufahamu kuwa klabu hiyo haina undugu wowote na Yanga.

"Unajua usajili wa Singida United ina leseni yake na namba zake,Yanga nae ana leseni yake na usajili wake,sasa sijajua huu ukaribu wa Singida United na Yanga umetoka wapi.Kama swala la walimu kocha yule ni mfanya kazi ambae anaweza kufanya kazi sehemu yeyote"alisema Sima.

Aidha Sima alisema kwamba ili kuwathibitisha uma wa watanzania kama klabu hiyo haina undugu na Yanga basi wasubiri hiyo siku ya mechi itakayowakutanisha na Yanga hapo novema 4 mwaka huu.

Hata hivyo Sima amewataka mashabiki wa timu hiyo kuendelea kukemea vikali habari hizo ambazo zina lengo la kuidhohofisha Singida United.

No comments