SIMBA KUWAFUATA MBEYA CITY WIKI HII

Kikosi cha timu ya Simba Wiki hii kinataraji kuanza safari ya kulekea Mbeya kwa ajili ya kujiwinda na pambano lao la ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Mbeya City hapo siku ya jumapili.

Mratibu wa timu ya Simba,Abasi Ally ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT.COM kwamba wamepanga kwenda mapema kutoka na hali ya hewa iliyopo mkoani Mbeya ambayo ni baridi tofauti na jiji la Dar es salaam.

Alisema kwamba kati ya alhamisi au ijumaa kikosi cha timu hiyo kitaanza safari ya kuelekea Mbeya tayari kupambana na Mbeya City.

No comments