YANGA YAANZA MAZOEZI YA KUWAKABILI SINGIDA UNITED

Kikosi cha timu ya Yanga leo hii kimeanza mazoezi kwa ajili ya kujiwinda na pambano lao la ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya Singida United hapo siku ya jumamosi ya novemba 4 mwaka huu.

Afisa Habari wa Yanga,Dismas Ten ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT.COM kwamba leo hii wachezaji wamefanya mazoezi ya Gym kama ilivyo utaratibu wa mwalimu na kesho wataendelea kufanya mazoezi ya uwanjani.

Alisema kwamba kuelekea katika mchezo wao dhidi ya Singida United maandalizi yako vizuri na jambo la faraja ni kurejea kwa wachezaji wao wote ambao walikuwa majeruhi.

No comments