TFF YATHIBITISHA KILIMANJARO HEROES KUSHIRIKI MICHUANO YA CHALLENGE

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limethibitisha kushiriki kwa timu ya Tanzania bara Kilimanjaro Heroes kwenye michuano ya Challenge inayotarajiwa kufanyika nchini Kenya kuanzia novemba 25 hadi desemba 9 mwaka huu.

Katibu mkuu wa TFF,Wilfred Kidao amesema kwamba kutokana na umuhimu wa michuano hiyo pamoja na nafasi ya Tanzania katika balaza la michezo la Afrika mashariki na kati CECAFA si jambo jema kwa Kilimanjaro kushindwa kushiriki michuano pasipo sababu ya msingi.

Kidao alisema kwamba kutokana na uwepo wa michuano hiyo ya Challenge,ratiba ya michezo ya ligi kuu ya Tanzania bara inatarajiwa kufanyiwa mabadiliko kwani awali ratiba hiyo ilipangwa pasipo kufuata tarehe ya michuano hiyo.

Alisema kwamba TFF na bodi ya ligi ilishindwa kupanga ratiba kwa kufuata kalenda ya michuano hiyo kwa sababu  kwa muda mrefu mashindano hayo yalishindwa kufanyika na pia kulikuwa hakuna dalili za kufanyika kwa mwaka huu.

No comments