ENOCK BELLA AVUNJA UKIMYA

Baada ya kukaa kimya kwa muda bila ya kutoa ngoma yoyote tangu kusambaratika kwa kundi la Yamoto Band,leo hii msanii aliyetokea kwenye kundi hilo Enock Bella ametusogezea nyimbo yake mpya inayojulikana kwa jina la Sauda.

Bella ni miongoni mwa wasanii ambao walikuwa hawapewi nafasi ya kufanya vizuri kwenye soko la muziki baada ya kundi la Yamoto Band kuvunjika ingawa mmiliki wa kundi hilo  Said Fella hajaweka wazi juu ya mustakabali wa kundi hilo.

Sababu kubwa ambayo iliwafanya wadau wa mziki kushindwa kumpa nafasi ni kutokana na mfumo wa uimbaji wa kutumia sauti ya besi,hivyo wengi wao walidhani kwamba huenda asingeweza kutoa ngoma kali akiwa peke yake.

Lakini kwa wimbo wake huu mpya unaojulikana kwa jina la "Sauda"nina imani utamrejesha kwenye hadhi yake ya awali kwani ni miongoni mwa nyimbo nzuri na imeanza kupokelewa vizuri na wapenzi wa muziki.

Bonyeza video kuisikiliza ngoma yake hapo chini.

No comments