SIMBA WAIANDIKIA BARUA TFF KUPINGA WAAMUZI
Uongozi wa klabu ya Simba umeliandikia barua shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF kueleza malalamiko yao juu ya waamuzi kushindwa kuwatendea haki katika mechi zao za ligi za ligi kuu ya Tanzania bara.
Mkuu wa idara ya Habari na mawasiliano wa klabu ya Simba,Haji Manara alisema kwamba barua hiyo wameiandikia TFF pamoja na bodi ya ligi huku pia nakala wakiiwasilisha kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ili watambue malalamiko yao.
Manara alisema kwamba waamuzi hao wameshindwa kutafasiri vyema sheria 17 za soka hasa katika mechi zao tatu za mwisho walizocheza dhidi ya Mbao FC,Stend United pamoja na mahasimu wao wa jadi Yanga.
Alisema kwamba katika mechi hizo waamuzi walionyesha dhuluma ya wazi kwa klabu ya Simba kwani maamuzi yaliyotolewa yalikuwa ni ya utata pamoja na kuwanyima penati ambazo zilikuwa za wazi.

Post a Comment