SIMBA YAAMUA KUMPLEKA MAHAKAMANI PIUS BUSWITA

Uongozi wa klabu ya Simba umepanga kumpleka mahakamani mchezji Pius Buswita baada ya uongozi huo kukasirishwa na kauli zake ambazo anaendelea kuzitoa kwenye vyombo vya habari.

Mkuu wa Habari na mawasiliano wa klabu ya Simba,Haji Manara ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwamba klabu hiyo imepanga kumpleka mahakamani mchezaji huyo ili aweze kurejesha fedha zao na pia vyombo vya sheria vichukue jukumu lao la kisheria kuhusiana na kauli zake anazozitoa.

Manara alisema kwamba klabu hiyo ilikuwa na nia ya kufanya uungwana wa kuachana na jambo hilo kwa sababu mchezaji alishafungiwa mwaka mmoja lakini sasa swala hilo limeanza kuzungumzwa tofauti ikionekana Simba imemuonea mchezaji.

Alisema kwamba klabu ya Simba ilikuwa na nia hata ya kukaa mezani na klabu ya Yanga ili kumsaidia mchezaji aendelee kucheza mpira lakini jambo hilo kwa sasa linaonekana kuwa gumu kutokana na baadhi ya watu kuchochea kwa makusidi ili ionekani Simba imetenda kosa.

No comments