MTIBWA SUGAR WAITISHA MWADUI FC

Wakata miwa wa Manungu wamejinasibu kufanya vizuri katika mchezo wao dhidi ya Mwadui FC,hapo siku ya jumatano mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara unaotarajiwa kupigwa Turiani huko mkoani Morogoro.

Afsa Habari wa Mtibwa Sugar,Thobias Kifaru alisema kwamba kikosi cha timu hiyo kinaendelea na maandalizi na mchezo huo katika block za miwa na dhamira yao msimu huu ni kurejesha heshima ya Mtibwa Sugar.

Alisema kwamba Mwadui FC,wanafahamu kuwa walishawahi kufungwa kwa jumla ya mabao 4 kutoka kwa wakata miwa hao wa Manungu hivyo anaamini wimbi hilo la ushindi linaendelezwa upya.

No comments