SAMATA AWASILI KATIKA KIKOSI CHA TAIFA STARS

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars,Mbwana Samata tayari ameshalipoti kambini kuungana na wenzake kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaopigwa septemba 2 mwaka huu dhidi ya Botswana.

Afsa Habari wa TFF,Alfred Lucas alisema kwamba mbali ya Samata,mchezaji mwingine anaecheza soka la kulipwa nje ya nchi aliyewasili ni pamoja na Elias Maguli.

Lucas alisema kwamba leo hii usiku wanatarajia kumpokea mchezaji Simoni Msuva ambae nae ni miongoni mwa wachezaji walioitwa na kocha mkuu wa timu hiyo Salum Mayanga.

Alisema kwamba kwa upande wa utawala,maandalizi kwa ujumla kuelekea kwenye mchezo huo wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya FIFA yako vizuri na amewaasa watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye pambano hilo ili kuwapa hamasa wachezaji wa timu hiyo ya Taifa.

No comments