MAYANGA ASEMA STARS IPO KAMILI KUIVAA BOTSWANA

Kocha mkuu wa timu ya Taifa Stars,Salum Shabani Mayanga amesema kwamba kikosi chake kimejipanga vyema kuwakabili Botswana hapo kesho katika mchezo wa kirafiki uliopo kwenye kalenda ya FIFA.

Mayanga alisema kwamba kiujumla hali ya kambi iko vizuri na mazoezi kwa upande wao yameenda vyema hivyo kwa maandalizi ambayo wameyafanya anaamini kikosi hicho kitapata matokeo mazuri katika mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Alisema kwamba katika kikosi cha timu hiyo ameweza kumuongeza mchezaji Abdlnasir Azizi anaecheza soka katika kituo cha Barcelona ya Hispania.

"Abdulnasir anaecheza kwenye kituo cha watoto cha Barcelona kwa sasa yupo mapumziko,hivyo nikaona nivyema nimuongeze kwenye kikosi na kesho nitakuwa nae na pia itakapobidi ikitokea nafasi nitampa nafasi kwani amefanya mazoezi na wenzake tangu jana jioni"alisema Mayanga.

Nae nahodha msaidizi wa Taifa Stars,Himid Mao alisema kwamba upande wa wachezaji wa timu hiyo ya Taifa Stars wao wamejipanga kikamilifu kuhakikisha wanachomoza na ushindi kwenye pambano hilo linalotarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu.

No comments