MAYANGA AMUONGEZA EMMANUEL MARTIN

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" Salum Mayanga amemuongeza winga wa timu ya Yanga Emmanuel Martin katika kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Botswana.

Afsa Habari wa TFF,Alfred Lucas ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kuwa Mayanga ameamua kumuongeza kikosini Martin baada ya kubaini kuwa wachezaji wawili wa timu hiyo ya Taifa kutokuwa na uwakika wa kujiunga na wenzao kwa kipindi hiki.

Lucas alisema wachezaji hao ambao hawana uwakika wa kujiunga katika kambi ya timu ya Taifa ni Morel Ergenes na Simoni Msuva.

Alisema kwamba kati ya wachezaji hao Msuva ana asilimia 50 ya kuwasili nchini baada ya kuwepo kwa mikakati ya kushughulikia swala lake la pasipoti ya kusafilia ambayo imeonekana kuwa ni ndogo hivyo anahitaji kubwa zaidi.

Kuhusu Morel anaecheza soka nchini Ureno,Lucas alisema kwamba kwa upande wake huyo mchezaji hana uwakika wa kuwasili hapa nchini kwa asilimia mia moja kwani kulikuwa hakuna mawasiliano mazuri kwa nchi na nchi.

Stars kwa sasa iko katika maandalizi ya kujiwinda na mchezo wa kirafiki ulio katika kalenda ya FIFA ambao mechi hiyo itapigwa siku ya septemba 2 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

No comments