ASHANTI WAHARIBU MIPANGO YA SIMBA ILI KUCHEZA NA YANGA

Wakati klabu ya Simba ikitangaza kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Hard Rock ya kisiwani Pemba hapo kesho,mchezo unaotarajiwa kupigwa katika uwanja wa Uhuru,nao ungozi wa timu ya Ashant United umesema kwamba kikosi chao hapo kesho kwenye uwanja huo wa Uhuru watashuka dimbani kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Yanga.

Msemaji wa timu ya Ashant United Adam Kinyogoli alisema kwamba kwa upande wao kama Ashanti United maandalizi yako vizuri kwa ajili ya pambano hilo ambalo ni mahususi kwa timu kujiandaa na michezo ya ligi daraja la kwanza.

Kinyogoli alisema kwamba licha ya Simba kutangaza kuwa na mechi ya kirafiki katika uwanja huo wa Uhuru hapo kesho kwao hilo hawalitambui,kwani wao wamefuata taratibu zote za kuomba uwanja hivyo mechi yao ya Yanga itachezwa kunako mishale ya saa kumi jioni kwa saa za Afrika mashariki.

No comments