GF TRUCKS YAIDHAMINI MBAO FC

Mkurugenzi wa Mtendaji kampuni ya GF Trucks & Equipment Imrani Karmali  na  Mwenyekiti wa Mbao Fc Solly Zephania Njashi wakionyesha hati ya makubaliano ya Mkataba  ikiwa ni mkataba wa udhamini wa timu hiyo kwa mwaka mmoja wenye thamani ya Milioni 140 sambamba na basi la wachezaji.

Kampuni ya Trucks and Equipment Ltd imeanza kutanua wigo wa masoko yhake katika soko la Tanzania hasa kanda ya Ziwa baada ya leo hii kusaini mkataba wa kuidhamini timu ya Mbao Fc ya mkoani Mwanza.

Kampuni hiyo imeridhishwa na maendeleo ya timu hiyo na kuamua kuwapatia udhamini kwani hawajawahi kushiriki katika udhamini wa soka kwa Kiwango cha ligi kuu.

Mkataba huo uliosainiwa mbele ya waandishi wa habari leo katika ofsi za TFF zilizopo Karume Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Imrani Karmali alisema kuwa mkataba huo ni wa kihistoria kwani unaenda kuleta na kukuza  maendeleo ya mpira wa miguu nchini.

Karmal alisema kuwa, madhumuni makubwa ya mkataba huo ni kukuza vipaji vya mpira wa miguu na wanatarajiwa kuisaidia Mbao Fc kufikia malengo yao msimu huu, " tunafahamu usafiri umekuwa ni tatizo kwa klabu nyingi ndogo za Ligi Kuu na hicho kimetupelekea kuanza na basi msimu huu ambapo katika mkataba wa milioni 140 utajumuisha sambamba na basi hilo la wachezaji lenye thamani ya milioni 70,".

"uwezo waliouonesha katika ligi kuu na hata kuingia fainali ya kombe la FA ulituhamasisha kuifuatilia kwa ukaribu sana  na tuna imani kwa msaada wetu Mbao itaendelea kufanya vizuri na si hao tu bali hata ajira kwa vijana zitaongezeka,"alisema Karmali.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Mbao Fc, Solly Zephania Njashi yeye kwa upande wake ameusifu mkataba huo na kusema kuwa utazidi kuleta chachu ya maendeleo katika klabu yao na hata kupunguza gharama za mahitaji kwa wachezaji ukizingatia timu hiyo bado ni changa.

Njashi ameishukurui kampuni ya  GF Trucks & Equipments  kwa mkataba huo na kuwaahidi mashabiki na wapenzi wa Mbao Fc ya Ilemelea mkoani Mwanza kuwa mwaka huu wataendelea kufanya vizuri na kuendelea kusalia katika Ligi kuu ya Tanzania bara msimu ujao.

 Baada ya kusaini mkataba huo, kampuni ya  GF Trucks & Equipments iiliwakabidhi mfano wa jezi zitakazovaliwa na timu ya Mbao tayari zikiwa zimeshaweka nembo ya kampuni hiyo.
 Mwenyekiti wa Mbao Solly Zephania Njashi akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuingia makubaliano ya udhamini wa mkatabwa mwaka mmoja na na kampuni ya GF Trucks & Equipments wenye thamani ya Milioni 140, kushoto ni Mkurugenzi wa Mtendaji kampuni ya GF Trucks & Equipment Imrani Karmali 
 Afisa Masoko wa Kampuni ya  GF Trucks & Equipments Kulwa Bundala akizungumza na wanahabari baada ya kuingia mkataba na timu ya Mbao Fc wenye thamani ya Milioni 140 kwa mwaka mmoja.
Mkurugenzi wa Mtendaji kampuni ya GF Trucks & Equipment Imrani Karmali  na  Mwenyekiti wa Mbao Solly Zephania Njashi wakionyesha jezi za Mbao zitakazotumikia mwaka huu.


Mbao Fc ni miongoni mwa timu ambayo imeonyhesha ushindani wa hali ya juu katika msimu uliopita baada ya kuzizuia baadhi ya timu kongwe za Simba na Yanga katika mechi za ligi kuu ya Tanzania bara na pia kufanikiwa kucheza fainali ya kombe la FA dhidi ya Simba.

Huu unakuwa udhamini wa pili kwa timu hiyo ambapo uongozi kupitia kwa mwenyekiti wake umedai kuwa bado unaendelea na mchakato wa kusaka wadhamini wengine ambao wataendelea kuisapoti timu hiyo.

No comments