TFF KUWACHUKULIA HATUA WALIOPANGA RATIBA YA LIGI KUU

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limepanga kuwachukulia hatua wataalamu wa ratiba ambao wamehusika kupanga ratiba ya ligi kuu ya Tanzania bara msimu wa mwaka 2017/18.

Kaimu katibu mkuu wa TFF,Wilfred Kidao alisema kwamba uongozi wa shirikisho hilo umeamua kuchukua jukumu hilo baada ya kubaini wataalamu hao wameshindwa kupanga vizuri ratiba ya ligi hivyo Rais wa TFF,Wallace Karia ametoa agizo kwa mtendaji wa bodi ya ligi achukue jukumu la kuwachukulia hatua wale wote waliohusika na swala hilo.

Kidao alisema kwamba ratiba hiyo imeanza kuwa na dosari mapema tu baada ya kuwepo kwa mwingiliano na mechi zilizopo kwenye kalenda ya FIFA na kupelekea ligi kusimama ili kupisha timu ya Taifa icheze mechi ya kirafiki iliyo kwenye kalenda ya FIFA.

Alisema kwamba baada ya kuwepo kwa jambo hilo TFF imetoa agizo kwa uongozi wa bodi ya ligi kuiangalia upya ratiba hiyo ya ligi na pia imeteua kikosi cha watu wa nne ambacho kitakuwa na jukumu la kuifanyia marekebisho ya msingi ratiba hiyo ambayo hayataleta athari katika ligi hiyo.

No comments