MASHABIKI YANGA WATOA LAWAMA KWA WAAMUZI

Mashabiki wa Yanga wametoa lawama kwa waamuzi waliochezesha mechi ya ligi kuu ya Tanzania bara iliyowakutanisha Yanga na Lipuli FC ya mkoani Iringa baada ya timu hizo kufungana kwa bao 1-1.

Mmoja wa mashabiki hao aliyetambulisha kwa jina la Gres Tadeo alisema kwamba waamuzi wote waliochezesha mechi hiyo ya ligi kuu ya Tanzania hawakufuata sheria 17 za mpira wa miguu.

Alisema kwamba waamuzi hao wameshindwa kubalansi muda wa mchezo kwani mara nyingi wachezaji wa Lipuli walikuwa wanajiangusha mara kwa mara lakini dakiki ambazo zimeongezwa hazikupaswa kuwa dakika 4.

Hata hivyo mashabiki hao wameliomba shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,kuliangalia upya swala la waamuzi ambao wengi wao wanashindwa kufuata sheria 17 za soka.

No comments