HAYA NDIO MAAMUZI YA TFF JUU YA WACHEZAJI OBREY CHIRWA NA KASEKE

Kamati ya nidhamu ya TFF imewaachia huru wachezaji Obrey Chirwa na Deus Kaseke baada ya kamati hiyo kubaini kuwa wachezaji hao hawakupaswa kupewa adhabu ya kusimamishwa.


Makamu mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya TFF,Peter Elam alisema kwamba kamati hiyo baada ya kupokea uteteza kwa wachezaji hao na kupata ushahidi wa picha ya mnato imebaini ni mchezaji pekee Simon Msuva ndie aliyekuwa na makosa baada ya kumuangusha mwamuzi wa mechi husika.

Alisema kwamba kamati hiyo itamuandikia barua ya onyo kali mchezaji Simon Msuva kwa kitendo chake ambacho alikifanya licha ya kuwa tayari alishaanza kutumikia adhabu ya kosa hilo ikiwemo kukosa kucheza baadhi ya mechi.

Wachezaji hao kwa pamoja wakati wanaitumikia timu ya Yanga msimu uliopita walisimamishwa na kamati ya masaa 72 baada ya kuonekana wamemuangusha mwamuzi katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara uliowakutanisha Yanga na Mbao FC.

No comments