MKWASA AJINASIBU KUWAFUNGA KAGERA SUGAR HAPO KESHO

Uongozi wa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara timu ya Yanga,umesema kwamba kikosi cha timu hiyo kimejiandaa vyema kuwakabili Kagera Sugar hapo kesho katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara unaotaraji kupigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Katibu mkuu wa mabingwa hao Charse Boniphace Mkwasa alisema kwamba wachezaji wote wako vizuri na kila mmoja ana hamasa ya kufanya vyema kwenye pambano hilo ambalo linataraji kuwa na ushindani zaidi kwa pande zote.

Mkwasa alisema kwamba wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na tahadhari kubwa kwani dhamira yao ni kushinda ili wajijengee mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wa ligi kuu.

Aidha alisema kwamba wachezaji wote wako vizuri ispokuwa Donald Ngoma ambae yeye yuko nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu lakini kwa asilimia kubwa wachezaji ambao walikuwa majeruhi kwa wakati huu wanaendelea vizuri.

No comments