ZANZIBAR YATANGAZA SILAHA NZITO ZA MAANGAMIZI RIADHA HUKO TANZANIA BARA .
Na sleiman ussi zanzibar
Kufuatia mashindano ya riadha ya Afrika ya mashariki na kati yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es salaam, chama cha riadha Zanzibar kimetangaza wachezaji watakao iwakilisha Zanzibar katika mashindano hayo
Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika tarehe 13/14.05.2017 katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kwa vijana wenye umri chini ya miaka kumi na saba ambao kwa Zanzibar itawakilishwa na Rosemary Gustafu Kazija, Zaina Ally, Othmani Hassan Nsimai, Asma Ayubu Yussuph, Omari Bakari Ally, Abdullatif Murtaza na Omar Bashir.
Viongozi ambao wataambatana na wachezaji hao katiksa kuiwakilsha Zanzibar katika mashindano hayo ya Afrika mashariki na kati ni katibu Nyambui,Mwenyekiti Abdulhakim Cosmas, Makam mwenyekiti Mbarouk,Meneja wa timu Muhidini Yasin ambapo pia msafara huo utaambatana na waamuzi watakaochezesha mashindano hayo.
Timu hiyo inatarajiwa kuondoka tarehe 12 mwezi huu na kutarajiwa kurudi tarehe kumi na sita ya mwezi huu wa tano katika mwaka wa 2017.
Hata hivyo wadau wa Zanzibar wameombwa kuipa sapoti timu hiyo kwa hali na mali ili ifanikiwe kuwakilisha vyema visiwa hivyo vya Zanzibar.
Post a Comment