CHAMA LA WANA LATOA ONYO KWA WAAMUZI

Uongozi wa kikosi cha timu ya Stend United ya mkoani Shinyanga umesema kwamba kwa wakati huu wapo kwenye maandalizi kabambe kuhakikisha wanachomoza na ushindi kwenye mechi yao ijayo dhidi ya Simba hapo siku ya ijumaa.

Msemaji wa timu hiyo Deo Kaji Makomba alisema kwamba wanaamini kikosi chao kitapata ushindi mbele ya Simba ili waendelee kuwepo kwenye nafasi yao ya sita katika msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Makomba pia amewataka waamuzi watakaochezesha mchezo huo kufuata sheria 17 za soka na kuacha kasumba ya kuzipendelea timu kubwa za Simba na Yanga.

"Niwaombe waamuzi watakaochezesha pambano letu watende haki,kwani mara nyingi waamuzi wetu wanakuwa na mahaba kama si mapenzi kwa vilabu viwili vya Simba na Yanga lakini naamini wakichezesha kwa haki basi chama la wana litaibuka na ushindi"alisema Makomba.

No comments