AFRIKA LYON WAPO KAMILI KUWAVAA MAAFANDE WA RUVU SHOOTING

Kocha mkuu wa timu ya Afrika Lyon,Charse Otieno amesema kwamba baada ya kushindwa kufanya vizuri kwenye mechi yao iliyopita mbele ya Simba kwa sasa nguvu zao wamezielekeza kwenye mechi yao ya kesho dhidi ya maafande wa Ruvu Shooting.

Otieno alisema kwamba wanatambua kuwa hawapo kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi hivyo ni lazima washinde kwenye mechi hiyo ili wajinusuru na janga la kushuka daraja.

Afrika Lyoni ipo nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara ikiwa na alama 31 baada kushuka dimbani mara 28.

No comments