SERENGETI YAONGEZA NEEMA KWA TIMU YA TAIFA

Kampuni ya bia ya Serengeti imesaini mkataba mpya wa kudhamini Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa stars  kwa miaka mitatu wenye jumla ya thamani ya shilingi billion 2.1.

Akiongea wakati wa utiaji saini wa mkataba huo Raisi wa TFF,Jamali Malinzi ameishukuru kampuni hiyo akiamini kwamba italeta chachu ya maendeleo ya mpira wa miguu hapa nchini.

Amesema kwamba fedha hizo ni muhimu kwa wakati huu kwani timu ya Taifa inaelekea kwenye ushiriki wa mashindano mbalimbali ikiwemo kuwania tiketi ya kufuzu fainali za kombe la dunia.

No comments