HATU YA 8 BORA LIGI KUU SOKA YA ZANZIBAR KUANZA RASMI SIKU YA JUMAMOSI HII..

Na Sleiman Ussi Zanzibar .
Hatua ya 8 bora ya ligi kuu soka ya Zanzibar inatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake siku ya  Jumamosi ya Mei 13, 2017 kwa kupigwa michezo miwili katika Viwanja viwili tofauti.

Katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba wataanza Kizimbani dhidi ya Okapi saa 10 za jioni ambapo Kisiwani Unguja katika Uwanja wa Amaan watasukumana JKU dhidi ya Zimamoto saa10:00 za jioni.


Jumapili ya Mei 14 itaendelea tena kwa kupigwa mchezo kati ya Mwenge dhidi ya Jamhuri saa 10:00 za jioni katika Uwanja wa Gombani huku katika dimba  Amani Unguja kutakuwa na mtanange mkali wa kukatana shoka wa watani wa jadi kati ya timu ya Jang’ombe boys wakioneshana kandanda dhidi ya Taifa ya Jang’ombe saa 2:00 za usiku.

No comments