MOHD YUSSUFU APANGA KUISAIDIA LIPULI FC

Na sleiman ussi zanzibar .
Mlinda mlango mahiri wa timu ya Lipuli  FC  ya mkoani Iringa ambayo imepata tiketi ya kucheza ligi kuu ya Tanzania bara kwa msimu ujao Mohd Yussufu,amerudi kisiwani Zanzibar kwa kwajili ya likizo maalumu waliopewa na walimu wao kabla ya kurejea tena katika timu yake.

Mohd alisema kwamba yeye akiwa kisiwani humo anaendelea kujifua na mazoezi makali ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara ili ajiweke fiti kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.

Mlinda mlango huyo aliyewai kuitumikia timu ya Chuoni ya Zanzibar ambayo inashiriki ligi kuu ya Zanzibar alisema kwamba anaamini mazoezi hayo yatampa tija ya kufanya vizuri katika msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara,kwani dhamira yake ni kuisaidia vyema timu yake ya Lipuli.

Katika hatua nyingine alielezea juu ya ushindani uliopo kati ya ligi ya Zanzibar na Tanzania bara,ambapo alisema kwamba ligi ya Tanzania bara ina ushindani zaidi hii inatokana na vilabu vingi kuwa na udhamini tofauti na Zanzibar.


No comments