ZFA WATAKIWA KUWALIPA WAAMUZI MADENI YAO

Na Sleiman Ussi Zanzibar .
Kamati ya Waamuzi Visiwani Zanzibar kupitia Mwenyekiti wao Issa Ahmada Hijja “Jogoo” amesema wamejipanga vyema kusimamia sheria 17 za soka hasa katika hatua ya 8 bora ya Ligi kuu soka ya Zanzibar ambayo inatarajiwa kuanza rasmi kesho Jumamosi.

Alisema wamejipanga vyema kulinda heshma yao na kila timu ipate haki yake lakini pia amewaomba ZFA kuharakisha kuwalipa madeni yao wamuuzi ambayo wanadai.

“Tumejipanga vyema  wamuuzi na hatuna wasi wasi wowote na vijana wangu kwenye hatua hii ya 8 bora, tulimaliza ligi ya Kanda kwa amani na usalama na tunategemea kuchezesha 8 bora ipasavyo, zaidi tunawaomba ZFA wafanye hima hima kuwaona Vijana wangu ambao bado hawajaonana nao kwa vile tuna deni letu ambalo bado halijalipwa”. Alisema Jogoo.

Hatua ya 8 bora ya ligi kuu soka ya Zanzibar inatarajiwa kuanza kesho Jumamosi ya Mei 13, 2017 kwa kupigwa michezo miwili katika Viwanja viwili tofauti.

Katika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba wataanza Kizimbani dhidi ya Okapi saa 10 za jioni ambapo Kisiwani Unguja katika Uwanja wa Amaan watasukumana JKU dhidi ya Zimamoto saa10:00 za jioni.

Jumapili ya Mei 14 itaendelea tena kwa kupigwa mchezo kati ya Mwenge dhidi ya Jamhuri saa 10:00 za jioni katika Uwanja wa Gombani huku Amani Mjini Unguja kutakuwa na homa ya Jiji la Jang’ombe kati ya Taifa ya Jang’ombe dhidi ya Boys saa 2:00 za usiku.

No comments