TFF;YANGA HAINA HOJA YENYE MASHIKO YA KUTAKA MECHI YAO ICHEZWE SAA 12 JIONI

Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini TFF,limesema kwamba hakuna taarifa za mabadiliko yeyote juu ya muda wa mchezo utakaowakutanisha mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania bara Yanga na wagonga nyundo wa Mbeya timu ya Mbeya City.

Afisa Habari wa TFF,Alfred Lucas ameiambia MWANDIKE.BLOGSPOT kwama taarifa za mechi kuchezwa saa 12 za jioni sio rasmi ispokuwa hayo ni maombi yaliyopo kwa upande wa Yanga.

Alisema kwamba maombi hayo yanaweza kukubaliwa au kukataliwa lakini kiujumla hadi kufikia sasa hakuna mabadiliko yeyote juu ya mchezo huo utakaopigwa siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Taifa.

Aidha alisema kwamba hata hoja inayoelezwa na klabu ya Yanga kuwa siku hiyo kuna mashindano ya riadha ya vijana kwenye uwanja huo hayana mashiko kwani mashindano hayo ya riadha yatafanyika asubuhi na wala sio jioni wakati wa mechi hiyo.

No comments