SIMBA IPO KAMILI KUIVAA STEND UNITED

Uongozi wa klabu ya Simba,umesema kwamba kikosi cha timu hiyo kipo tayari kupambana na Stend United hapo kesho katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara unaotaraji kupigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mjumbe wa kamati ya utendaji wa klabu ya Simba,Said Tully alisema kwamba kikosi cha timu hiyo kilianza maandalizi tangu siku ya pili baada ya mechi yao iliyopita dhidi ya Afrika Lyoni hivyo anaamini kuelekea kwenye mchezo huo anaamini kikosi hicho kitapata ushindi.

Alisema kwamba kwa sasa malengo yao ni kushinda mechi zao ambazo zimesalia na hawaangalii wapinzani wao wamefanya nini kwa bado wana matumaini ya kuwa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara msimu huu.

No comments