JKT RUVU KUMENYANA NA DAR CITY

Kikosi cha timu ya JKT RUVU ya Kibaha mkoani Pwani hapo kesho kinataraji kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Dar City,mchezo unaotaraji kupigwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Afisa Habari wa JKT RUVU,afisa mteule daraja la pili Costantine Masanja alisema kwamba kwa sasa timu inaendelea na mazoezi ya mwisho katika uwanja wa makao makuu ya JKT Mlalakua tayari kwa kujiwinda na michezo mitatu iliyobaki ya ligi kuu ya Tanzania bara.

Masanja alisema kwamba kikosi hicho kinaendelea kuongozwa na mkurugenzi wa ufundi Abdalah Kibaden ambapo kwa upande wake amedai kuwa maandalizi yanaenda vizuri kwa ajili michezo hiyo, ambapo mechi ya kwanza kati hizo tatu wataanza kumenyana Toto Africans itakayopigwa jijini Mwanza.

Maafande hao wa JKT RUVU,bado wanaendelea kusalia kwenye nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi kuu ya Tanzania bara wakiwa na alama 23 baada kucheza mechi 27.

No comments